Malipo ya Sh100 kila mwezi kuwezesha Wakenya kupata huduma bora hospitali

Featured on Taifa Leo on Saturday, July 15, 2017

Kenyans can now access affordable health services from private hospitals by saving Sh100 monthly in their M-Tiba accounts.

KWA miaka mingi, Wakenya wemekuwa hawana bima ya afya kutokana na mapato yao ya chini. Kwa sababu hii ilikuwa ni vigumu kupata matibabu bora katika vituo vya afya na hospitali kubwa za serikali na kibinafsi. Lakini sasa kwa kuwekeza Sh100 pekee, katika huduma ya M-Tiba kwenye simu, Wakenya wanaweza kulipia huduma za afya katika hospitali za kibinafsi na kupata matitabu bora.

Huduma hii ya kuwekeza pesa kwa simu kwa ajili ya matitabu pekee, ilianzishwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Carepay, kampuni ya maduka ya kuuza dawa ya PharmAcess na kampuni ya Safaricom. Wanaowekeza pesa katika huduma hii wanaweza pia kuzitumia kununua dawa katika maduka mengi yaliyosajiliwa chini ya mpango huu.

Kulingana na afisa mmoja wa kampuni ya Carepay Bw Steve Maina, kuna hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 kote nchini zinazotumia huduma ya M-Tiba.

"Kwa sasa tuna zaidi ya wateja 350,000 wanaotumia huduma hii kufadhili matibabu yao na watoto wao. Haibagui kamwe, inashughulikia watu wote wanaowekeza na ambao hawawezi kupata huduma za bima kutoka kampuni na mashirika mkubwa ya bima," asema Bw Maina.

Afisa huyu anaongeza kuwa lengo la kubuni M-Tiba, ilikuwa ni kuwezesha Wakenya kuwekeza pesa kwa ajili ya matibabu pekee.

Read the full article

We are an award winning team